Kampuni mpya ya simu Tanzania ya Viettel imetangaza nafasi za ajira nyingi na watu wanaruhusu kuomba kuanzia sasa. Wafanyakazi wanaohitajika ni wa vitengo vya rasilimaliwatu, sheria, fedha, uhasibu, masoko, uchumi, mipango, takwimu, uwekezaji, ugavi, usafirishaji, utunzaji wa vifaa, umeme, simu, teknolojia ya habari na mawasiliano, biashara, utawala na uhusiano wa umma.
Maombi yanatakiwa kutumwa kwa barua pepe, nayo ni viettelrecruiter @gmail dot com, ukiwasilisha ombi lako la kazi basi watakutumia fomu maalumu.
Nafasi ni nyingi sana kwani wanaitaji wafanyakazi buku 2 na ni kwa maeneo mbalimbali nchini.
Kazi ni kwako! | Kuifahamu Viettel Zaidi BOFYA HAPA
No Comment! Be the first one.