Warning: Illegal string offset 'custom_css_post_id' in /home/content/n3pnexwpnas01_data01/25/3112425/html/wp-includes/theme.php on line 905

Clean Master: Moja App Muhimu Kuwa Nayo

na Mhariri Mkuu 1

Sambaza upendo 🙂
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  

clean-androidKuna muda mwingi simu zinakuwaga nzito na utendaji wake wa kazi unaathirika sana, zinakuwa na joto sana na muda mwingine ata zinaweza zikawa ata zinazima pale chaji ikiwa safi tuu. Na hapa ndio app hii ya Clean Master inakuja.

Ata pale unapokuta nafasi ya uhifadhi (storage) imepungua kwenye simu au tableti yako ya Android, Clean Master itakuonesha ni nini hasa kinakula nafasi na kukusaidia kufuta vitu usivyoitaji.

Utakapofungua app ya Clean Master itakuonesha kupitia michoro (graphs) ni nini kina kula nafasi kwenye simu au memori kadi yako. Pia itakuonesha ata nafasi inayoshikiliwa uchafu (cache) uliotokana na oparesheni za apps ulizonazo. Kupitia chaguo rahisi la ‘Clean’ yaani safisha, app inasaidia sana kwani hauitaji kuwa na ujuzi mwingi sana, katika utumiaji wa app hii kwa muda mrefu haijawahi kuharibu au kuathiri app au mafaili yeyote muhimu.

Ata pale simu inapokuwa inaanza kushika joto app hii itakuonesha ni apps gani zinasababisha joto hilo, na inakupa chaguo la kuzifunga apps hizo.

cleanmaster

Kwa kiasi kikubwa app hii itasaidia kuongeza maisha ya simu yako. Kushusha bofya hapa – Google Play

Facebook Comments

Sambaza upendo 🙂
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  

ZINAZOHUSIANA

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com