Wakati iOS na Android zimekua kwa kiasi kikubwa na zina vipengele mbalimbali vinavyo fanana lakini kile kikubwa cha kuwatofautisha ni keyboard.
Simu za android ziliwezesha keyboard kutoka kwa watu wengine ambao waliweka application (keyboard) hizo katika google playstore, Apple hawakufanya hivyo toka mwanzo. Tangia iOS 8 itoke Apple walifungua mlango kwa watengenezaji wa keyboard hii imechangia mpaka baadhi ya watengenezaji wa keyboard katika Android kutengeneza zile za iPhone na iPad.
Kazi kubwa imefanyika na Teknokona kutofautisha mchele kutoka kwenye maharage. Zifuatazo ni keyboard nzuri zaidi katika iOS.
Fleksy
Keyboard ya Fleksy ni nzuri sana na inatoa huduma katika vipengele vingi kama vile kuotea, kumalizia maneno, na kurekebisha maneno (gestures, auto-correction, text prediction, and size options). Inaweza pia kukusoma jinsi unavyandika katika barua pepe (E-mail) zako na mitandao ya kijamii.
Kama maelezo hayo hayatoshi Fleksy bado inatoa huduma ya vitu kama emoji, GIFs na uwezekano wa kuandika kwa kutumia mkono mmoja. Kitu kimoja tuu ambacho haifanyi ni kuandika juu ya kioo ili maandishi yatokee. Lakini kwa dola moja tuu ya kimarekani sidhani kama unaweza lalamika.
Minuum
Minuum ina bei kubwa kuliko Fleksy. lakini inafanya vitu ambavyo keyboard nyingine haziwezi fanya. Kikubwa ni kwamba ina uwezo wa kuficha keyboard yote kwa chini kabisa na kutengeneza mstari mmoja chini ya skrini. Kwa kutumia vipengele vyake vya kuotea na kumalizia maneno bado inaweza kukusaidia kuandika maneno kwa kugusa skrini yako tuu.
Wengine wanaweza pata shida kujua kuitumia mara moja tuu, lakini kila kitu ni kujifunza tuu ili kuelewa. Pia hii keyboard ya minuum inakusaidia kuweza kuongeza kamusi yako kwa kutumia maneno yako mwenyewe. Na kama unapenda sana emoji Keyboard hii itafanya yote hayo kwa ajili yako.
SwiftKey
SwiftKey ni keyboard nzuri na mbadala kwa jaili ya iOS pia ni ya bure. Tangia mwanzo ilikua inapendwa sana na watumiaji wa Android.
Sio tuu inaweza otea maneno yako na kumalizia baadhi ya meneno kwa ajili yako pia itasoma namna au jinsi unavyo tuma meseji kwa katika mitandao ya kijamii (Facebook, Twitter, Gmail, Evernote, na akaunti za namba za simu ) ili kukusaidia katika kuandika.
Pia keyboard hii ni moja kati ya zile nyingi ambazo zinaweza kukuwezesha kuandika kwa kutumia mkono mmoja.
Swype
Kama jina linavyoonyesha Swype ilikua ni moja kati ya zile keyboard za mwanzo katika Android ambayo inamuwezesha mtu kuandika juu ya skrini ili maneno yatokee. Tangia Apple waruhusu watu kutengeza keyboard kupitia mlango wa nje, Swype ikabisha hodi katika iOS.
Wakati keyboard zingine zinafanya juu chini ili ziweze otea maneno yako au kumalizia maneno yako, Swype inafanya kila namna ili mtumiaji wake aweze kuandika neno analo lihitaji pale anapolihitaji na hichi ndio kitu ambacho kinafanya vizuri, tena vizuri sana.
Pia ina kamusi kwa ajili ya kuongeza maneno na pia inakupa nafasi ya kuchagua mionekano (‘theme’) mabali mbali
ThemeBoard
Kubwa kuhusu hii keyboard ni kwamba imejikita zaidi katika ‘theme’ ndio maana ikaitwa ‘ThemeBoard’. Keyboard hii ni bure na pia inatoa mionekano mbali mbali ya bure lakini vitu vingine bomba vitaku gharimu kitu kidogo
Themeboard haina mambo ya ajabu sana kwani itatoa huduma sawa na SwiftKey au Fleksy.
Jinsi Ya Ku ‘Install’ Keyboard Katika iOS
- Shusha Keyboard unayoitaka katika AppStore
- Katika iPhone au iPad Ingia katika menu ya setting kisha nenda General -> Keyboard -> Add New Keyboard
- Chagua ile Uliyo ishusha
- Keyboard ikitokea katika App mfano WhatsApp bonyeze kialama cha dunia kile kisha chagua ile unayoitaka
No Comment! Be the first one.