Katika siku za hivi karibuni, kampuni za Apple na Google zimeonesha dira mpya kwa viunganishi vya vifaa vya kielekroniki kwa kuitambulisha USB-C kama kiunganishi pekee kwenye kompyuta zao mpya.
USB-Aina ya C (au USB-C kwa kifupi) ni kiwango kipya na aina mpya ya kiunganishi kinachoifuata USB 3.0. Kiunganishi cha USB-C kimevumbuliwa kwa ajili ya kuchukua nafasi ya viunganishi vingine kwa karibu kila kitu. Pamoja na hilo, USB-C inapunguza ukubwa wa vichwa na kuongeza urahisi wa kukichomeka kwenye vifaa. Pia, inasafirisha chaji na data nyingi zaidi.
Kiunganishi cha USB-C kinaweza kutumika kwa kuunga vifaa vingi ikiwemo laptopu, simu, skrini za kompyuta na runinga. Jambo hili litaondoa ulazima wa kumiliki waya za aina mbalimbali kwa ajili ya vifaa vyako vya kielektroniki.
Utengenezaji wake ni ushirikiano wa kampuni kadhaa ikiwemo Microsoft, Intel, HP, Renesas Electronics na Texas Instruments kama inavyoelezwa na ukurasa huu. Ingawa kampuni hizo zimeungana kutengeneza kiwango hiki kipya cha USB- C, kiwango hiki ni huru, yani hakimilikiwi na mtu, kampuni au taasisi yoyote na hivyo, kampuni yoyote duniani inaweza kuitumia kutengeneza viunganishi vya USB-C.
Faida zake:
- USB-C ina uwezo wa kuchaji vifaa vya aina nyingi, ikiwemo simu, tabiti na laptopu.
- Inamaanisha hakutakuwa na haja ya kubeba mabonge ya adapter za laptopu tuliyoyazoea. Inavyosemekana, itawezekana kuchaji kompyuta, simu na tabiti kwa waya wako mmoja.
- Kuna uwezekano wa kuangalia video kutoka kwenye simu yako kwenye tv kiurahisi.
- Ina uwezo wa kutumika kuwasha skrini za kompyuta na tv kwani inapitisha umeme wa kutosha.
- USB- Aina ya C inauwezo wa kusafirisha data hadi GB 10 kwa sekunde, ambayo ni mara 3 zaidi ya USB 3.0!
- Itafanya kompyuta kuwa vidogo zaidi kwani mashimo ya kuunganisha vifaa vingine yatakuwa machache zaidi.
- USB-C inatabiriwa kudumu kwa miaka mingi kama ilivyokuwa kwa USB.
Mategemeo:
Kama kawaida katika mabadiliko ya viwango, itachuka muda kwa USB-C kufunika USB ya sasa na itatubidi tupitie vifaa vingi na hata vinuganishi vya mseto kabla ya kukutana na kiunganishi hiki. Tegemea kuanza kutumia USB-C katika simu na laptopu mpya zinatoka hivi karibuni.
No Comment! Be the first one.