Ni ukweli usiofichika kuwa makampuni makubwa katika tasnia ya teknolojia yanatengeneza hela nyingi sana. Licha ya kwamba tunaweza jua kiasi cha pesa wanachotengeneza baada ya wao kutuambia katika ripoti zao
Tunaweza wenyewe kuangalia ni kiasi gani wanatengeneza kwa sekunde – ndio kuna watu wanaingiza hela kila baada ya sekunde – kila siku
Mtandao wa Portas Group ambao unatoa taarifa za kibiashara unafanya kazi ya ziada kwa kuangalia makampuni makubwa mtandaoni ili kujua yanatengeneza kiasi gani cha pesa.
Mtandao unaonyesha majibu moja kwa moja kati ya faida zinazotengenezwa na mapato ya makampuni ya kiteknolojia ukijumuisha Apple, Alphabet, Microsoft, Facebook, Amazon, YouTube na Netflix. Faida hizi ni kwa kila sekunde….
Katika dakika moja mtandao unasema kuwa makampuni yote katika ukurasa huo yanapata mapato ya dola 141,780 kwa pamoja na asilimia 50 ya mapato hayo yanaenda kwa kampuni la Apple.
Hata hivyo hii isikushangaze juu ya Apple, Ripoti zinasema kuwa kampuni la Apple liliripoti mapato yake kuwa bilioni 51.5 katika ripoti ya mwezi septemba 26, 2015 na vile vile ikasema kuwa faida yake ambayo ishatolewa ushuru ni bilioni 11.1 za kimarekani.
Kutoka Katika data za mtandao wa portas group zinasema kuwa kampuni la Apple kwa kukadiria linatengeneza dola 60,000 kwa dakika.
Makampuni kama Facebook na Yahoo yanapata mapato yake kutoka kwenye simu na komyuta (Intanet). Licha ya makampuni mengi kuonekana yanapata faida iliyonona mitandao kama Pandora, Yelp na Twitter bado wanajikongoja katika kupata mapato.
Mtandao huu unatusaidia kujua makampuni makubwa duniani katika teknolojia yanapata mapato kiasi gani na hata faida zake.
Kujionea Mikwanja Hiyo Ingia … https://portasgroup.com/internet-giants/
No Comment! Be the first one.