Instagram ina maboresho kadha wa kadha, mara kwa mara kumekua na maboresho au vipengele vipya ambayo wanakuja navyo.
Sasa ni zamu ya biashara za karibu, inaelekea awali watumiaji wa mtandao huo walikua wanatapa shida kutambua biashara ambazo zipo karibu yao kwa namna moja au nyingine.
Toleo hili jipya ni kwamba litakua linafanya kazi kwa kuweza kutoa ramani ambayo moja kwa moja itakua uwezo wa kukuonyesha maeneo mbali mbali na biashara mbalimbali ambazo zinapatikana katika maeneo hayo.
Sasa utafikia vipi ramani hiyo, kama kawaida mtu anaweza akawa ame’post kitu chake na kwa juu pale akawa ameweka anuani ya sehemu. Unaweza ingia kuangalia eneo (sehemu) hiyo kwa kuibofya
Ukifanya hivyo moja kwa moja utaenda kwenye ramani hiyo, ukishakua ndani ya ramani ndipo unaweza kuona biashara mabli mbali zilizo karibu na hata unaweza zunguka zunguka katika ramani hiyo.
Hiyo sio njia pekee ya kuliwezesha hili pia unaweza amua kuingia kwenye ramani kwa kuingia katika eneo la kutafuta (search) na kisha ukaandika kitu unachotaka tafuta kama vile biashara, eneo n.k
Ukishaandika unachotaka kutafuta, kubali kukitafuta na kisha katika majibu ingia katika eneo la places hapa moja kwa mota utapelekwa kwenye ramani hiyo.
Unaweza ukaona mambo mengi sana ukiwa kwenye ramani, sehemu kama za migahawa, maduka ya vitabu, sehemu za starehe na maeneo mengine mengi unaweza kuyaona kwa kutumia mbinu hii.
Vile vile unaweza kuhifanyi (save) baadhi ya maeneo ambayo ungependa uyapitie hapo baadae, maeneo haya utaweza kuyafikia kwa kuingia katika ukurasa wako (profile) na kisha kwenda katika eneo la Saved.
Chanzo: The Verge
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje? Je ulikua unatumia huduma hii ili kutambua maeneo mbalimbali?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.