Miaka miwili iliyopita kama ungeniuliza kama Snapchat itakuwa maarufu kwa kiasi hichi nisingekuwa na uhakika, ila tayari app hii inakua kwa kasi siku hadi siku…na sasa imefikisha takribani wastani wa watumiaji milioni 150 kwa siku.
Data zinaonesha mtandao wa kijamii wa Twitter una wastani wa watumiaji milioni 140 kwa siku na hivyo hii inaonyesha tayari Snapchat imeshaiacha nyuma Twitter.
Data za wastani wa watumiaji wa app hiyo kwa siku imevujishwa na mmoja wa wafanyakazi wa mtandao huo wa kijamii kwenda kwa mtandao/gazeti la habari la Bloomberg.
Kupata picha tuu ya kwa kiasi gani ukuaji huu ni wa kasi sana kumbuka;
- Mwezi Disemba 2015 Snapchat ilikuwa na wastani wa watumiaji milioni 110 kwa mwezi – hivyo katika miezi mitano wameweza ongeza zaidi ya watumiaji milioni 50 kwa siku.
- Twitter ina miaka 10 wakati Snapchat ina takribani miaka 5 tuu
Pia data zinaonesha Snapchat itaendelea kukua kwa kasi zaidi ukilinganisha na Twitter ambayo ukuaji wake umekuwa mwendo wa kobe kwa miezi mingi sasa.
One Comment
Comments are closed.