Ilivyotoka saa janja tuliona kama ni kitu cha ajabu mpaka tukaja kizoea (mimi nimeshazoea) lakini uzuri wa teknolojia ni kwamba unachokiona leo ni cha ajabu kesho utakiona ni cha kawaida sana
Lenovo wao wamemua kuleta teknolojia ya kiatu (viatu) janja. Viatu hivi ni spesheli kwa wale wanokimbia huku vikiwa na mbwembwe kibao za kiteknolojia
Baadhi Ya Vitu Ambavyo Kiatu Janja Hicho Kinaweza Fanya
> Kutumika Katika Kuongoza Gemu – Ili kuendena na wakati. Kampuni imeamua kugawa mamlaka katika viatu janja hivyo ya kuweza kuongoza michezo mbalimbali katika simu janja. Kwa msaada wa viatu hivi wachezaji wanaweza wakacheza gemu kwa kwenda kushoto au kulia, kuruka na kuweza kufanya mambo mengine mengi ndani ya gemu husika. Kumbuka pia hata kwa yale magemu ya kucheza (Dancing Games) viatu hivi vinaweza vikawa ndio chaguo sahihi
> Hifadhi Ya Taarifa Za Afya – Viatu hivi sio tuu kwa ajili ya kutembelea tuu, pia vinasimamia swala zima la Afya ya mtumiaji. Viatu hivi vina skana ya 3D ambayo inapatikana katika soli inatumika katika kuangalia Afya ya mtumiaji. Skana hiyo ina uwezo wa kugundua kiwango (asilimia) cha mafuta cha mwili, kiasi cha jasho linalotiririka wakati wa mazoezi na uzito wa mtu.
> Viatu Hivi Vinawaka Kwa Chini – Viatu hivi vina taa za mfumo wa LED ambazo zinapatikana katika upande wa chini kabisa wa viatu hvi. Hii ni msaada mkubwa sana kwa wale wanaofanya mazoezi (sana sana ya kukimbia) katika nyakati za usiku. Kingine ni kwamba inasemekana taa hizi zinaendana na mdundo wa muziki pale unaposikiliza muziki.
Kizuri kuhusiana na kiatu hiki ni kwamba kila mtu anaweza akavaa maana kina muonekano wa kawaida tuu. Yaani sio lazima uwe unafanya mazoezi ndio uweze kuvaa kiatu hiki bali hata kwa matumizi ya kawaida unaweza ukakivaa.
Lenovo haikuingia ndani sana kuhusiana na kiatu hiki. Haikusema ni malighafi gani ilitumia, bei bado haikuwa wazi.
Angalia Video Hii Kujionea Zadi Kuhusu Kiatu Janja Hiki