Inakadiriwa kwamba ifikapo 2018 Tanzania itakuwa na Helikopta ambayo imetengenezwa hapa hapa nyumbani, ndege hii inatengezwa katika chuo cha ufundi Arusha ambapo ni mabingwa wa kuunda vifaa mbali mbali vya moto.
Gazeti la kiingereza la Daily News likiripoti habari hii limesema kwamba hatua za mwazo za mradi huu zimekwisha kamilika ikiwamo michoro na mambo mengine ya kibunifu. Kukamilika kwa Helikopta hii kutafungua njia kwa uzalishwaji wa ndege nyingine nyingi za kama hii kwani hii ndiyo kama mfano.
Akimuelezea Katibu mkuu wa wizara ya elimu Muhandisi Abdi Mjema ambaye ndiye anayeongoza mradi huo amesema kwamba wanashamirisha sera ya viwanda ya Raisi John Magufuli kwa kuleta Helikopta ya kwanza iliyotengenezwa hapa nyumbani.
Ingawa kwa kiasi kikubwa kazi imekwisha kamilika lakini bado timu ya wahandisi hao inawasiliana na mamlaka ya usafiri wa anga Tanzania kwaajiri ya kupata ruhusa ya kufanyia majaribio ndege hiyo.
Timu ya wahandisi ambao wanaifanyia kazi ndege hiyo ni pamoja na muhandisi Abdi mjema na muhandisi Adisai Msongole. Ingawa bado ni mapema mno kujua ni kwa kiasi gani mafanikio ya mradi huu yatahamasisha ukuaji wa teknolojia lakini Teknokona tunajiunga na wadau wengine kuwatakia kila la kheri wahandisi hawa ili waweze kufanikiwa.
Tupe maoni yako juu ya habari hiii na pia kama una swali ama maoni usisite kutuandikia.