Ripoti zilizopo ni kwamba kampuni ya Huawei inatengeneza Programu-endeshaji yake yenyewe kama vile tahadhari kama mambo yakienda kombo baina yao na Google ambao wanamiliki program-endeshaji ya Android.
Mpaka sasa Huawei ni kampuni Kubwa la tatu kwa utengenezaji wa simu janja duniani kote. Simu za Android zinatumia programu-endeshaji ya Android.
Ni sawa kabisa kuwa simu janja nyingi siku hizi zinatumia Android lakini hili bado haliwaogopeshi Huawei. Pia kumbuka kuna makampuni kama vile Apple ambao wanatengeneza simu janja za iPhone wana OS ya kujitegemea wao kama wao na wanafanya vizuri sana katika soko la simu na kompyuta kwa ujumla
Ripoti imetoka ikisema kuwa timu kutoka Huawei inatengeneza Os ya simu huko nchini Sweden kwa kushirikiana na wafanyakazi wa zamani wa kampuni ya Nokia
Jambo hili inabidi lisikushangaze kabisa hivi ushawahi kufikiria kama makampuni haya mawali (Huawei na Google) yakigombana nini kitatokea? Inamaana mamilioni ya simu kutoka Huawei yatakuwa hayatumiki? Kumbuka Google ndio Android!
Hvi ni vizuri kwa kampuni yeyote kuwa na plani nyingine kama jambo kama hili litatokea haswa kwa kampuni kubwa kama Huawei
Kampuni kwa sasa ni moja kati ya makampuni kubwa sana duniani katika soko la simu janja. Moja kati ya lengo lake kubwa kwa sasa ni kuweza kuweka saini na kampuni lolote kubwa la mtandao huko marekani kama vile AT&T, Verizon, T- Mobile au Sprint
Pia kumbuka katika masoko ambayo yameendelea huwa watoi sifa kubwa kwa makampuni ambayo yametoa bidhaa ambayo bado kwa namna moja au nyingine bado inatumia kipengele kingine kutoka kampuni nyingine katika bidhaa hiyo (Yaani Huawei Inatumia Android)
Kama simu hiyo ingekuwa inajitegemea kwa kila kitu mpaka Os basi katika ingepata sifa kedekede katika masoko ambayo yameendelea.
Kwa mfano wakati simu za BlackBerry na Nokia zilisifiwa sana wakati zilipokuwa zinatumia OS zake zenyewe. Watu wengi waliposikia Blackberry wanarudi na OS ya Android walikohoa kwanza kabla ya kukubaliana na matokeao.