Mtandao wa kijamii wa Youtube ambao unajihusisha na maswala ya video ambao pia unamilikiwa na kampuni ya Google umeweka wazi kuwa umeanzisha huduma ya ‘Live Stream’
Huduma hiyo kwa sasa ni kwa wale watu wenye majina makubwa kama vile Wasanii na wanasiasa. Hapo baadae kila mtu atapata nafasi ya kuitumia huduma hii kwa Youtube wana mpango wa kuhakikisha kuwa kila mtu anaifurahia hii huduma.
Huduma hii kutoka Youtube itakuwa ikiminyana vikali na huduma kama vile Facebook Live kutoka Facebook na Periscope Kutoka Twitter.
Lakini pia kumbuka Youtube ni kampuni ambayo imebobea sana katika maswala ya video hivyo basi hii inaweza ikawafanya wasipate changamoto kubwa sana na ya kutishia kutoka kwa makampuni mengine yanayotoa huduma ambayo inafanana na hii
Kwa kuwa huduma hii inapatikana katika App ya Youtube katika simu basi hata muonekano wake utakuwa unafanana kabisa na video zingine za mtandao huu. Ukitaka kutafuta video utaweza kuitafuta kwa kawaida tuu kwa kuiandika katika kiboksi cha kutafuta (search) au ukaiona katika mapendekezo (recommended)
Siku hizi Video zinanachukua sehemu kubwa sana, App nyingi zinajikita sana katika kuhakikisha zinakuwa na kipengele cha video. App kama Snapchat imepata umaarufu kwa video zake fupi ambazo zinapotea mara tuu unapoziangalia au kwa masaa 24
Kwa Youtube hili nalo ni jambo zuri licha ya kwamba litawaongezea mapato lakini pia wanarahishisha namna ya mawasiliano baina ya watu na watu.