Google licha ya kushangaza watu wengi na teknolojia zao zilizojaa ubunifu wa kutosha bado kampuni inazidi kuhakikisha kuwa inazidi kujiboresha
Sasa wameamua kuja na teknolojia nyingine, Wameweza kuweka mkonge wa intaneti chini ya bahari. Mkonge huu una urefu wa maili 5600 na unaunganisha marekani na japan kupitia maji
Kebo hiyo ya faiba inaweza ikasambaza data za terabaiti (terabits) 60 kwa sekunde ambayo ni sawa sawa na Megabaiti Milioni 60 kwa sekunde (60M Mbps)
Kwa sasa uhitaji wa Wavuti (internet) umeongezeka kwa kiasi kikubwa sana na hii ni kwa sababu siku hizi vifaa vingi vinakuwa vinatumia wavuti ili kuhakikisha vinapata vitu mbalimbali kupitia mtandao.
Karibia wavuti zote za nchi zilizoendelea zinapatikana kwa kupitia kebo (mikonge) ambayo ipo chini ya bahari. Inavyosemekana mikonge ile ambayo ina teknolojia ya kuwezesha kupita katika bahari ndio inakuwa ina uwezo mkubwa katika kuwasilisha huduma yake ya intaneti
Kipindi cha nyuma huduma nyingi za wavuti zilikuwa zinapatikana kwa kutumia msaada wa Satellite
Mkonge huo utaunganisha maeneo ya Los Angeles, San Francisco, Potland na Seattle na ukijumuisha maeneo mawili huko Japan
Google hawapumziki hapo tuu bado wapo katika mchakato wa kutengeneza mkonge ambao utaunganisha Florida na Brazil ambao unategemewa kumalizika mwishoni mwa mwaka huu.
Mikonge kama hii ili kukamilika inahitaji mamilioni ya pesa, hapo Google itakuwa imetoa mamilioni ya pesa. Japokuwa vyanzo vinasema kuwa Google hawakuwa wenyewe katika kuhakikisha jambo hili lainafanikiwa. Inasemekana walipata baadhi ya misaada kutoka katika makampuni mengine ya Asia