Kampuni ya Apple kwa sasa inatuhumiwa na mwanaume mmoja kutoka Florida, ambae analalama kuwa kampuni hiyo imemuibia ubunifu wake wa mwaka 1992
Jamaa huyo anasema ubunifu wake huo ndio umepelekea mpaka Apple wakatengeneza simu za iPhone, iPod na iPad. Kwa kifupi ni kwamba jamaa anadai ameibiwa ubunifu huo tena ukiwa katika Mchoro (michoro)
Jamaa huyo anaejulikana kama Thomas S. Ross anaomba alipwe fidia ya bilioni 10 za kimarekani na kampuni hiyo (Apple) – pesa hizo ni nyingi sana – kidogo hii inaweza ikawa inawashangaza wengi, lakini kwa namna moja au nyingine kesi hii ipo!
Thomas alikiambia kituo cha Guardian kuwa anajua anapigana vita kubwa sana kwani analishtaki moja kati ya kampuni kubwa kuliko yote duniani na katika vita hiyo yuko yeye peke yake, lakini hataishia hapo kwani haki ni haki tuu!
“Sikuweza kuuifikisha ubunifu wangu mbali zaidi kwani nilikuwa masikini, mpaka sasa bado ni masikini. Na pia sikuwa mzuri katika kuwafuata wawekezaji na kuwauzia mawazo yangu” – Alisema Thomas
Michoro ambayo Thomas aliichora ni ya kifaa cha kumuwezesha mtu kusoma au kuchora, maarufu kama ERD (Electronic Reading Device). Thomas anadai kifaa hicho ni chanzo cha kutengenezwa kwa iPhone, iPod na iPad.
Kumbuka iPhone ndio simu ya kwanza kuja bila ya kuwa na keyboard ya kutachi (zingine zilikuwa na ile ya kubonyeza)
Thomas kwa upande wake anasema mwaka 1992 ambapo aliandaa ubunifu huo na kuuhifadhi kwa njia ya michoro hakuweza kuulipia ili kuusajili uonekane wakwake kwani hakuwa na pesa kipindi hicho. Hali hiyo ilipoendelea kitengo cha marekani cha ubunifu na hakimiliki kiliamua kuachana (kwani haukulipiwa ili uwe unamilikiwa na mtu mmoja) na ubunifu huo.
Kingine cha kushangaza kutoka kwa Bw. Thomas ni kwamba hataki kuishia katika kuomba fidia ya bilioni 10 za kimarekani bali pia amesema kuwa anataka inabidi awe analipwa aslimia 1.5 (1.5%) katika thamani ya mauzo ya iPhone yanayokuja
Kwa sasa kampuni la Apple linaingia mapato ya bilioni 3.5 kwa mwaka, sasa hapo pata picha jamaa akiwa anachukua asilimia 1.5 tuu.