Kampuni ya Apple ina fikiria kuinunua kampuni nyingine ya muziki (Ule wa ku’stream’) yaani Tidal ambayo inamilikiwa na msanii Jay Z
Kumbuka tayri kampuni la Apple linatoa huduma sawa na Tidal kupitia Apple Music. Hapo mtu unaweza ukajiuliza ni jambo gani linapelekea kampuni hilo kutaka kununua kampuni lingine ingawa kila huduma zao zinafanana.
Pengine labda Apple Music wakiangalia miaka kadhaa ijayo wanaona kabisa kuwa Tidal itakuwa ni tishia licha ya hivyo kumbuka mmiliki wa kampuni ya Tidal nae ni mwanamuziki (Jay Z) hii inamaanisha kuwa yuko karibu na wanamuziki wenzake
Kuwa karibu na wanamuziki wenzio ni rahisi sana kuwashauri kujiunga katika mtandao wako (Tidal). Tidal ilianzishwa mwaka 2014 na ilijikita katika muziki wenye kiwango cha hali ya juu. Na hivi karibuni ilipata mamlaka na vibali vya kuweza kuruhusu watu ku’stream’ nyimbo na albamu za wasanii wenye majina makubwa sana
Kwa mfano Albamu yote ya msanii Kanye West (Life Of Pablo) ilikuwa inapatikana tuu katika mtandao huo ambayo pia ili vunja rekodi ya Albamu inayouza sana kipindi ilipotoka. Kumbuka Kanye West ni mmoja kati ya wasanii wanaoongozaga kwa mauzo duniani kote
Jay Z alifanya hivyo makusudi ili kuhakikisha kuwa anachuana vikali na makampuni mengine ambayo yanaleta changamoto kwa Tidal. Makampuni kama vile Spotify, Apple Music ni changamoto kwa Tidal
Maongezi bado yanaendelea kwa sehemu zote mbili lakini pia usije ukashangaa kuwa dili halifanikiwi kwa sababu itategemea na utayari wa uongozi wa Tidal. Viongozi wa Tidal walipoulizwa kuhusiana na jambo hili walisema hizo ni fununu tuu.
Tangia Jay Z alipo inunua Tidal 2014 mpaka sasa Tidal imeongezeka thamani kwa kiasi kikubwa sana. Na hii imetokea baada ya Jay Z kufanya maboresho kadha wa kadha na pia ukiangalia ukaribu wake na wasanii wenye majina makubwa sana duniani
Ukiachana na Tidal na Apple Music, kampuni ya Spotify ambayo ndio inaongoza katika muziki ule wa Ku’stream’ yenyewe inalalamika kuwa Apple inaibania. Spotify wanasema Apple wanaleta figisu figisu katika App yao ambayo ipo katika soko la App Store kutoka Apple. Spotify pia inasema kuwa kampuni la App lilikataa kuwawezesha Spotify kusasisha (Update) App yao ya iOS
Chanzo: Wall Street Journal