Apple waungana na chuo kikuu cha Naples Federico II kuanzisha Academy (chuo cha mafunzo) kwa ajili ya waundaji wa iOS iliyochini ya Apple na kuzinduliwa mwezi Oktoba.
Takribani wanafunzi wapatao 200 watapata nafasi ya kuweza kujifunza jinsi ya kutengeneza apps kwa ajili ya programu endeshaji ya iOS inayotumika kwenye simu za iPhone na tableti za iPad. Mafunzo hayo yatadumu kwa zaidi ya miezi 10 ambapo yatashirikisha wataalamu kutoka Apple na chuoni hapo kuweza kuwafundisha wanafunzi hao.
Katika muhula wa kwanza wanafunzi wataweza kuongeza msukumo wa jinsi ya kuweza kutengeneza programu/apps kwenye iOS. Katika muhula wa pili wanafunzi hao wataenda mbali zaidi ya uundaji(coding) na kuweza kujua jinsi ya kuunda muonekano wa awali wa programu hiyo endeshaji.
Wanafunzi watakuwa wanajifunza katika makundi na binafsi (individually) na kutengeneza apps mbalimbali ambazo zitawekwa kwenye ‘App store’. App store inatoa ajira zaidi ya 75,000 nchini Italia, kwa hakika idadi hiyo itaongezeka baada ya wanafunzi hao kuhitimu mafunzo yao.
Ingawa Apple hawajasema ni nchi gani itakayofuata kuweza kuwa kuwa na academy kwa ajili ya kufundisha wanafunzi jinsi ya kutengeneza iOS, nchini India Aoole wana mpango wa ‘kudesign’ na kujenga kituo Hyderabad kitakachokamilika mwaka 2017.
Wanafunzi ambao watapenda kujiunga katika academy hiyo wanatakiwa kutuma maombi yao katika tovuti yao chuo na ni bure kwa wanafunzi kutoka bara la Ulaya. Scholarships zipo kwa baadhi ya wanafunzi na itajumuisha pesa kwa ajili ya kuweza kujikimu. Waombaji wote watapewa jaribio(test) ambayo itakuwa katika lugha za Kiingereza na Kitaliano.
Kwa mtu yeyote amabye angepnda kujiunga na programu hiyo itakayoanza mwezi wa 10 kwa ajili ya kufundisha anaruhusiwa kujiunga kupitia academy ya waundaji wa iOS.
Je, unadhani hii ni mbinu tu ya Apple kujipatia developers kiulani? Tuambie mawazo yako katika comment. Teknokona siku zote tunakuletea makala za kusisimua.
Vyanzo: Tech, times, MacRumors.