Google imezidi kujiongezea uwezo wake (ambao bado uko juu) na kujiweka katika hatua nzuri zaidi. Hii ni baada ya kampuni hiyo kuinunua kampuni ya Avanto
Avanto ni kampuni inayojihusisha na maswala ya video kwa ujumla. Yaani kampuni hii inajihusisha utoaji na utengenezaji wa programu spesheli za masuala ya kutengeneza video, kuihariri, kuhakikisha kuwa inawafikia watu waliokusudiwa kwa usalama na pia inatoa miundombinu ya kufanikisha ku’Stream’ video.
Avanto pia ni kampuni ya video yenye miaka nane na imekua ikitumiwa na makampuni mengi na makubwa kama vile NBCUniversal, Univision na Fox Sports
Kutokana na dili hilo kwa sasa kampuni ya Google ina uhakika wa kutoa huduma bora kabisa katika maswala ya Video ili kufikia matakwa ya makampuni ambayo yanahitaji huduma hiyo kwa kiwango cha hali ya juu
Avanto itaenda katika Google kwa ubora wake uleule hii ni ukijumuisha na ‘Live Streaming’, kuhadhiri/kutoa video, huduma ya matangazo n.k.
Google wameamua kuinunua Avanto kutokana na dhamira yao kwa wateja wao ambao wanajihusisha katika mitandao na ‘media’ tofauti tofauti. Hii itawasaidia wao kuweza kuendesha taarifa zao huku wakiwa wanajipunguzia mzigo mkubwa wa kazi
Mpaka sasa Google bado haijaweka wazi kuwa ni vipengele gani wataanza navyo katika huduma yake ya ‘Cloud Platform’ japokuwa wengi wanategemea kuwa baadhi ya vitu vya Avanto vitaanza onekana katika huduma hiyo hivi karibuni