Facebook Messenger imefikia moja kati ya malengo yake ya muda mrefu. Hivi sasa ina watumiaji bilioni moja kila mwezi
Kampuni ilitangaza jambo hili katika post ya blog, na iliwashukuru watumiaji wake sana ambao kwa namna moja au nyingine wameliwezesha kampuni kufikia hatua hiyo
Kumbuka Facebook Messenger itakuwa imefikia hatua za Facebook na WhatsApp ambao wote hawa wanafikisha watumiaji bilioni moja
Katika Facebook Messenger Haya Yanatokea
– Picha bilioni 17 zinatumwa kila mwezi
– Stika milioni 380 zinatumwa kila mwezi
– GIF milioni 22 zinatumwa kila siku
Na hii inamaanisha kuwa katika mtandao huo kuna mambo mengi mtu anaweza akafanya ukiachana na kuchati tuu. Kumbuka ndani ya mtandao wa Facebook Messenger mtu anaweza akatumia kama sehemu ya kujiburudisha kwa kucheza michezo (gemu) mbalimbali kama vile mpira
Kumbuka wakati ilipoanzishwa mwaka 2011 kulikua hakuna haja ya kuishusha katika vifaa vyetu yaani ilikua ni mpaka mtu mwenyewe aamue kuwa nayo.
Kwa mwaka 2012 na 2013 mtandao huo (Facebook Messenger) ikaanza kujitegemea yaani ilikuwa sio lazima mtu awe anatumia mtandao wa Facebook ndio awezo kutumia Messenger kwani watu waliweza kujiunga katika mtandao huo hata kwa kutumia namba za simu.
Mtandao huo ukawa unajitegemea kabisa kwa kila kitu. Messenger ikaanza kujiboresha zaidi kwa kuongeza vipengele mbalimbali kama vile uwezo wa kupiga na kupokea simu kuonyesha kama meseji zimesomwa au la
Moja kati ya kitu kikubwa kilichosaidia messenger kupata watumiaji wengi ni kile kitendo cha kujitoa katika App kubwa. Kumbuka hapo awali Facebook Messenger ilikuwa inapatikana ndani ya App ya Facebook. Mwaka 2014 watu walilazimika kuishusha App nyingine ya Facebook (Facebook Messenger) kama wanataka kuona na kujibu meseji zao wakiwa katika simu zao
Mwazoni watumiaji wengi wa mtandao wa Facebook hawakupenda jambo hili lakini ukifikiria sana hawakuwa na njia mbadala. Baada ya muda facebook walianza kuwatuliza watumiaji wao kwa kuongeza vipengele kadha wa kadha katika App hiyo
Mambo kama vile picha,video,GIF, stika uwezo wa kutuma na kupokea pesa na bila ya kusahau magemu ndani ya App ni moja kati ya vitu ambavyo viliwafanya watu kuweza kuacha kuchukia maamuzi ya Facebook kuifanya Messenger ijitegemee
Jinsi mtandao huo unavyotumiwa sana kwa sasa hivi hapa duniani ni wazi kabisa kama mtu atakuwa hatumi meseji za kawaida basi bila shaka atakuwa ndani ya mtandao huu