Uber ni moja kati ya kampuni kubwa duniani ambalo linaendesha biashara kubwa za usafiri. Sasa kampuni ya Uber inauza biashara yake ya china.
Na uzuri ni kwamba mnunuaji kashajulikana. Huyu si mwingine ni kampuni inayojulikana kama Didi Chuxing, ambayo nayo pia inajihusisha na biashara ya usafiri.
Kinachofanyika hapa ni kwamba kampuni hiyo ya Didi itanunua kazi za Uber za nchini China.
Kama ulikua hujui ni kwamba makampuni hayo mawili (kwa nchi ya china) yalikuwa na ushindani wa hali ya juu. Kwa kampuni ya Didi kununua kazi za Uber huko uchinani inamaanisha kutakuwa hakuna ushindnai kama ulivyokuwa awali.
Dili hili thamani yake ni dola bilioni 35 za kimarekani na pia kampuni ya Uber itakuwa na umiliki wa asilimia 5.89 kama hisa katika kampuni la Didi.
Kila kampuni itakuwa inatumia App yake kama kawaida ila uongozi katika pande hizo zote mbili itajuaa ni jinsi gani ya kufanikisha jambo hili.
Japokuwa Didi imeliteka soko la china lakini bado inashirikiana na makampuni mengine kadha wa kadha ili kuhakikisha wanatoboa katika mipaka ya china na kwenda katika nchi zingine.
China ina soko gumu sana tumeshashuhudia makampuni mengi yakifunga biashara zao kule na wengine wakifunga kabisa mfano, Yahoo (waliuza kwa Alibaba), eBay na sasa Uber wanauza kwa Didi.
Japokuwa Uber imeshindwa katika soko la china, kumbuka bado haijaondoka kule mikono mitupu na pia bado inaendelea kutanua mabawa yake katika nchi zingine nyingi duniani. Mwaka huu tulishuhudia ikiingia bongo na Afrika Mashariki kwa ujumla.