Kusahau password ni jambo linalowakuta wengi? Google inataka kukusaidia kutokumbuka password zako. Fahamu kuhusu Open YOLO!
Soma pia –
1. Jinsi Ya Kutengeneza Neno Siri (Password) Imara!
2. Makosa katika utengenezaji wa password za Simu na
Google wanaungana na kampuni inayomiliki app ya kusimamia nywila (Password manager) ifahamikayo kama Dashlane kuhakikisha watumiaji wa Android hawatakuwa na ulazima wa kukumbuka password zao katika kutumia (log in) katika apps mbalimbali.
Wamekuja na kitu kinaitwa Open Yolo – yaani ‘You Only Log In‘…wakimaanisha uta’login mara moja tuu katika simu yako na kisha katika apps zote unazotumia hautaulizwa tena masuala ya password.
Mpango (project) huo unahusisha makampuni mbalimbali yanayotoa huduma/apps zinazowasaidia watu kutengeneza na kuhifadhi passwords wanazotumia katika mitandao mbalimbali.
Apps/huduma za kuhifadhi na kusimamia passwords (password managers) kama vile Dashlane, LastPass na 1Password, zote zinakusaidia kusimamia masuala ya passwords zako na kupitia mpango wa Open Yolo basi haitajalisha huduma unayotumia hautalazimika kuingiza password.
Ingawa nia ya jambo hili ni zuri ila bado linaleta wasiwasi kiusalama kama mdukuzi akifanikiwa kuingia kwa kutumia mfumo huu..kwani huduma nyingi zinaweza athirika kwa wakati mmoja. Ila tuna uhakika Google tayari ashaliona hili na watakuwa wamejipanga vizuri kiusalama.