Magari yasiyotumia funguo (keyless remote) kutoka kampuni ya Volkswagen yapo katika hatari kubwa ya kudukuliwa mfumo wake wa kufunga(lock) na kuwasha gari.
Teknolojia inavyozidi kukua na ndivyo ambapo vitu vingine tunavyovitumia kila siku kama vile magari n.k navyo vinaboreshwa zaidi.
Lakini kwenye teknolojia na usalama kuna imani moja kuu ambayo ni kwamba kila unavyozidi kuboresha programu flani basi na ndivyo kazi ya kuhakikisha inakuwa salama kutoka kwa wadukuzi inavyozidi kuwa kubwa na ngumu.
Kundi la watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Birmingham wamechapisha taarifa inayoonesha waliweza kudukua rimoti za magari ya VW (Volkswagen) kwa kuwa eneo la karibu na mtu anaye bonyeza rimoti yake kwa ajili ya kufunga (lock) au kufungua (unlock) gari lake.
Inasemekana mtu aliyepanga kudukua na kutengeneza nakala nyingine ya rimoti za gari flani ataitaji tuu kuwa na eneo la karibu na kuweza kuingilia mawasiliano ya rimoti halisi na gari pale mtu anapolock au kuondoa lock.
Namba ya magari yanayoweza kuathirika ni mengi sana (milioni 100) kwa kuwa mfumo huo umetumika kwenye magari mengi sana kuanzia mwaka 1995 (familia yaani ‘Models’ za Audi, VW, Seat na Skoda).
Volkswagen wamesemaje?
Msemaji wa kampuni ya VW ameonekana kukubali matokeo ya watafiti hao kwani alipoulizwa kuhusu matokeo ya utafiti huo alisema matoleo yao ya magari ya sasa hayaathiriki na udukuzi huo akionekana kuepuka kuongelea yanayoathirika.
Je ni vigumu sana kudukua?
Inasemekana upatikanaji wa bei rahisi wa vifaa mbalimbali vya teknolojia ya kimawasaliano ya redio unarahisisha sana mtu yeyote mwenye ujuzi na nia ya kufanya udukuzi na uibaji wa magari hayo kufanikiwa.
Soma Pia
Uwezekano wa nywila yako Kujulikana kama unatumia Wireless Keyboard
Hacker ahukumiwa kifungo cha miaka 4 kwa kosa la kudukua siri za Jeshi la Marekani