Kuwa na tatuu (tatoo) mkononi inayoweza ku’control simu au kompyuta? Jambo liko kama kimuvi zaidi lakini tayari Microsoft na chuo cha MIT wanakuja na teknolojia hiyo. Fahamu kuhusu DuoSkin.
Watafiti wafanikiwa kutengeneza tatoo ya madini ya chuma (metallic) yenye uwezo wa kuendesha (control) simu, kompyuta au kifaa kingine chochote kilichounganishwa na tatuu (tatoo) hiyo.
Wanafunzi wa PhD wa chuo cha MIT (Michigan Institute of Technology) wakishirikiana kitengo cha utafiti cha Microsoft wamefanikiwa kutengeneza tatuu ya kwanza iliyotumia madini ya chuma.
Tatuu hiyo kwa sasa ni ya muda mfupi tuu, yaani ‘temporary’….
Utakapoivaa inageuza eneo la mkono wako kuwa kama eneo la kipanya cha mguso kwenye ‘laptop’. Na eneo hilo linalofunikwa na tatuu hiyo litaweza badilika rangi kulingana na joto la mwili wako.
Teknolojia kuu zilizotumika katika utengenezaji wa tatuu hizo ni pamoja na chip za NFC na LED.