Google wanakuja na programu endeshaji nyingine nje ya Android na Chrome OS. Programu endeshaji hiyo inayokwenda kwa jina la Fuchsia tofauti na Android na Chrome OS hii inajitegemea na haitatumia Linux.
Fuchsia ni ya nini?
Inasemekana programu endeshaji ya Fuchsia inalenga zaidi kutumika katika vifaa vingine vya kisasa kama vile friji, mifumo ya usalama, n.k na si kushindana na Android na Chrome OS kwenye simu na laptop.
Android na Chrome OS zinazotengenezwa na Google zitaendelea kuwepo ila wameona ni muhimu kuwa na programu endeshaji nyingine nyepesi kwa ajili ya kutumika kwenye vifaa janja vya kisasa.
Inaonekana Google wanachukua hatua kama zilizochukuliwa na Samsung, ambapo Samsung wanamiliki programu endeshaji ya Tinzen OS ambayo wanaitumia kwenye vifaa janja ambavyo wanaona hakuna ulazima wa kutumia Android nzima.
Android OS inazidi kukua na ukuaji wake unaifanya isifae sana kutumika katika vifaa nje ya Simu, Tableti, kompyuta n.k.
Vyanzo: AndroidPolice na mitandao mbalimbali