Huawei wametambulisha simu mbili hapo jana, Huawei Nova, na Huawei Nova plus. Simu hizi zinaonekana kuja kuleta ushindani katika soko la simu za bei ya kati, na pia kuzidi kukuza nafasi ya Huawei katika soko la simu duniani.
Kama majina yake ya yalivyo, ukitoa tofauti kadhaa baina ya simu hizi mbili, ukubwa ni moja ya tofauti kuu.
Hizi ni simu zenye muonekano wa simu za hadhi ya juu (hasa kutokana na kuacha kutumia plastiki),zikiwa pia na uwezo wa ngazi ya kati (mid range).
Sifa za Huawei Nova
- Ukubwa – inchi 5 (display – 1080p HD)
- Prosesa ya Snapdragon 625
- RAM ya GB 3
- Diski uhifadhi GB 32
- Kamera ya megapixel 12
- Kiwango cha betri cha mAh 3,020
- Bodi ya simu imeundwa kwa kutumia malighafi za alumini (aluminium)
Sifa za Huawei Nova Plus
- Ukubwa – inchi 5.5,
- Kamera megapixel 16
- Betri – mAh 3,340
Ukitoa tofauti hizo chache mengine yote yanafanana na uwezo ulio kwa Huawei Nova. Na simu zote zinakuja na toleo la Android 6.
Bei
Huawei Nova inategemewa kuuzwa kwa bei ya kati ya Tsh 970,000/= | Ksh 45,000.
Huawei Nova Plus kwenye Tsh 1,050,000/= | Ksh 48500/=... (tegemea chini kidogo au juu kidogo zikianza kupatikana nchini)
Zitafanikiwa?
Inaonekana Huawei wanajikita katika kuhakikisha wanabadilisha mtazamo wa suala la ubora kwa bidhaa zinazotoka nchini China kwa makampuni ya kichina. Huawei tayari kupitia simu zake za familia ya P, Huawei P, wamefanikiwa kuuza vizuri katika masoko ya ulaya na marekani.