Instagram inaondoa kipengele chake cha ramani katika App yake. Hii inamaanisha baada ya muda tutasahau kabisa kuona picha za watu wakiwa wame’tag’ maeneo ambayo wana’post’ picha hizo.
Instagram ishafuta huduma hiyo ya ‘map’ hata kwa baadhi ya watu hivi sasa, na plani yao ni kukiondoa kabisa kipengele hiko katika uso wa App yake.
Instagram walianza kuondoa kipengele hichi kwa baadhi ya watu wiki iliyopita lakini tangia hapo bado walikuwa hawajatoa taarifa kamili, muda kidogo ulipopita ndipo taarifa kamili zikatoka katika vyombo mbalimbali.
Sawa pengine mpaka sasa unaweza ukawa bado unaona kipengele cha ‘map’ katika picha zako lakini tegemea mabadiliko katika siku za usoni.
Wao Instagram wanasema kuwa wameamua kuondoa kipengele hicho kwani watu wengi wamekuwa hawakitumii hivyo wameona ni vyemu kukitoa kabisa.
Kumbuka kipengele hiki kilikuwa kinatumika kama huduma ya ‘Check In’ yaani kama vile mtandao wa FourSquare – hata facebook wana huduma kama hii tuu – ulivyo.
Pia msemaji wa Instagram alisema kuwa zoezi hilo zima la kuondoa kipengele hicho cha ‘map’ halitaathiri wale ambao wanafanya biashara matangazo katika mtandao huo. Ni wazi kuwa matangazo ya instagram yanategemea kwa kiasi kikubwa maeneo. Hilo halitawaathiri kwani bado instagram itakua na njia yake ya kuweza kupata maeneo hayo.
Kuna waliopokea vibaya jambo hili lakini kuna wengine hata hawajali. Lakini ni kweli kabisa hivi ukifikiria wewe mara ya mwisho kutumia huduma hii? Mimi nimeshasahau kabisa.
Niandikie sehemu ya comment hapo chini je hii wewe umeipokeaje? Au ndio imeshakuathiri. Ningependa kusikia kutoka kwako.