Warning: Illegal string offset 'custom_css_post_id' in /home/content/n3pnexwpnas01_data01/25/3112425/html/wp-includes/theme.php on line 905

Wezi wazima safari ya bajaji inayotumia Nishati ya jua Ufaransa

na Mato Eric 0

Sambaza upendo 🙂
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  

Safari ya miezi saba ya bajaji inayotumia umeme wa jua (solar), ambayo ilikuwa inatoka India kwenda hadi Uingereza, imesitishwa kwa muda baada ya wezi kuiba hati ya kusafiria ya dereva wa bajaj hiyo karibu na mji wa Paris.

Mhandisi Naveen Rabelli aliibiwa pasipoti na pochi yake eneo la Sarcelles, alipokuwa ameenda haja. Kwa sasa anasubiri kupata pasipoti mpya ndipo aweze kuvuka English Channel na kuhitimishia safari yake katika Kasri la Buckingham.

Bajaj yenyr kutumia umeme wa jua 'ilitakaswa' kabla yake kuanza safari India
Bajaj yenye kutumia umeme wa jua ‘ilitakaswa’  🙂 kabla ya kuanza safari India

bajaj-umeme-jua

Nia yake kuu ni kujaribu kuwahamaisha watu kutumia nishati mbadala. Safari hiyo ishachukua miezi saba sasa kutoka nchini India, na maandalizi yake yalichukua miaka minne.

Huwa analala kwenye bajaji hiyo anapokosa mtu wa kumpa malazi. Amefanikiwa kuweka pesa nyingi kwa njia hii. Amepitia Iran, Uturuki, Ugiriki, Bulgaria, Serbia, Austria, Ujerumani na Uswizi.

Bajaj ina kitanda na jiko la sola.
Bajaj ina kitanda na jiko la sola.

Mhandisi huyo alinunua bajaji hiyo $1,500 (£1,120)|Tsh 3,300,000 na akatumia $11,500|Tsh 25,300,000 kuifanyia ukarabati. Kwa sasa, bajaji yake inaweza kufikia kasi ya juu ya 60km/h (37 mph) na hutumia umeme unaotengenezwa na nishati ya jua.

Mhandisi muundaji wa bajaj ni  mkazi wa India lakini ni raia wa Australia na amekuwa akifanyia kazi kampuni ya kuunda magari ya kutumia umeme nchini India.

Vyanzo: BBC

Facebook Comments

Sambaza upendo 🙂
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  

ZINAZOHUSIANA

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com