Morogoro pengine itaweza kuepuka migogoro ya ardhi baina ya wafugaji na wakulima karibuni.
Hii ni baada ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na washirika kuanza kutumia teknolojia ya Drone katika kuharikisha upimaji wa maeneo mbalimbali mkoani humo.
Pamoja na kuitwa kisiwa cha amani Tanzania imekuwa ikitiwa doa na baadhi ya matukio ya mauaji yanayotokana na mapigano baina ya jamii za wafugaji na wakulima. Kwa muda mrefu hili tatizo limeshindwa kuzuiliwa pamoja na jitihada zote za serikali pamoja na wadau wengine.
Wakulima na wafugaji kimsingi wanagombana kwasababu hakuna mipaka mizuri ya kuzitenganisha jamii hizi ili zisiingiliane, hivyo kupunguza migogoro hii serikali ina pima na kuyagawa maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Changamoto katika zoezi hili ni kwamba kwa ukubwa na uhalisia wa maeneo mengi basi ingechukua siku nyingi kwa wapimaji kuyafikia na kuyapima, kutatua hili wizara itatumia Drones katika kufanya kazi ya upimaji umeripoti mtandao wa.
Teknolojia hii ya Drones itatumiwa na wizara kusaidia kupima maeneo kwa ustadi na usahihi zaidi lakini jambo la msingi ni kuongeza kasi la upimaji huu.
Drones zinauwezo wa kufanya kazi ambayo ingechukua muda mrefu kwa muda mfupi zaidi na pia kwa gharama za chini zaidi, pia kwa vijijini hatari ya drone hizi kugongana na ndege ni ndogo sanaa.