Baada ya kushuhudia tukio la kihistoria la kupatwa kwa jua lililotokea mwanzoni wa mwezi huu, leo usiku Tanzania itashuhudia pia tukio jingine la kupatwa kwa mwezi takribani wiki mbili tuu baada ya tukio la kupatwa kwa jua.
Tukio hili linategemewa kutokea usiku wa leo tarehe 16 huu na linategemewa kuendelea kwa karibu masaa matatu, tukio hili litaweza kushuhudiwa maeneo mengi ya Amerika, Afrika, Asia, Austraria na Ulaya tofauti na lililopita ambalo lilonekana maeneo machache ( hali iliyopelekea baadhi ya watu kufikiri kwamba ni amri ya serikali kwamba tukio hilo limetokea Mbeya ?????).
Safari hii tukio ni tofauti yaani ni Mwezi ndio umepatwa hivyo hautahitaji kifaa maalumu kwaajiri ya kushuhudia tukio hilo lakini kama utatumia darubini ama hadubini basi utaweza kuona tukio hili vizuri zaidi.
Tofauti na tukio lililopita ambapo Mwezi ulikuwa katikati ya dunia na Jua safari hii dunia ipo katikati ya mwezi hii inasabisha kivuli cha dunia kiangukie katika mwezi na kuufanya mwezi usiwe angavu kama ilivyo kawaida yake.
Christopher Columbus ambaye alikuwa mpelelezi wa kiitaliano aliwahi kutumia ujuzi wake wa mambo ya anga kupatiwa huduma baada ya kuwadanganya kabila moja kwamba mungu wake amekasirika ndio maana kauficha mwezi.