Samsung Galaxy Note 7 ni simu janja ambayo ni toleo jipya katika muendeleo wa familia ya Samsung galaxy Note. Imekuwa faraja kwa wateja waliokuwa wamenunua Samsung galaxy Note 7 ambazo zilipatikana kuwa na dosari baada ya muda fulani.
Simu ya Samsung Galaxy Note 7 iliodaiwa kuwa na betri zinazolipuka imeanza kubadilishwa Uingereza, soma zaidi.
Kampuni ya Samsung inataka wamiliki wa simu hizo walioathirika kuwajulisha waliowauzia, lakini wengi wa wafanyibiashara wa simu hizo wanasema tayari wanawasialiana na wateja wao moja kwa moja.
Wito umetolewa kwa wateja kupeleka simu hizo ili ziweze kubadilishwa haraka iwezekanavyo ambapo Samsung galaxy Note 7 zenye betri ya kijani zilikuwa salama kutumia.
Hata hivyo ni wateja wachache tu ndio wameweza kukubaliwa kubadilishiwa simu zao kutokana na baadhi ya wateja hao (waliokataliwa kubalishiwa simu zao) kununua simu hizo sehemu nyingine au walinunua kupitia mtandaoni (online).
Tangu simu hizo kupata matatizo mauzo yake yameshuka kwa 0.1% kuanzia mwezi Agosti kitu ambacho maka sasa kimesababisha hasara ya mabilioni ya dola duniani kote.
One Comment
Comments are closed.