Mmiliki wa Facebook, Mark Zuckerberg kwa kushirikiana na mkewe (Priscilla Chan) wameanzisha mpango kabambe ambao una lengo kubwa la kutibu magonjwa.
Mpango huu unaitwa ‘Chan Zuckerberg Initiative’ ambapo ndani ya mpango huu Mke wa Mark amesema kuwa atatumia dola bilioni 3 za kimarekani ndani ya miaka kumi na hii ikiwa ni moja kati ya hatua zake za kusaidia kutibu magonjwa ya binadamu.
Kwa sasa mpango huo (Chan Zuckerberg Initiative) unawekeza dola milioni 6 za kimarekani katika mradi unaojulikana kama Biohub. Biohub ni kitengo cha uchunguzi kinachojitegemea na kipo katika chuo kikuu cha California huko San Fransisco.
Kitengo hicho kimejikita katika kutengeneza na kugundua vifaa vipya ambavyo kwa namna moja au nyingine vitasadia au vitatumika katika kutibu magonjwa.
Chan kwa hisia alisema kuwa kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita yeye na mumuwe walikuwa wakiongea sana na wanasayansi, ukaichana na wale wenye majina makubwa na tuzo kadhaa pia waliongea hata na wale waliohitimu vyuoni.
Priscilla Chan anaamini maisha mazuri kwa watoto (kizazi kijacho) yanawezekana na wao (kizazi cha sasa) ndio kina jukumu la kuhakikisha kuwa wanakitengenezea mazingira mazuri kile kijacho na hii ikiwemo na kuwasaidia katika kutatua au kupata tiba za magonjwa kadhaa.
Lakini Priscilla Chan alisema kuwa hii haimaanishi kuwa hakuna mtu atakaye umwa bali kwa ana imaani watoto wetu na watoto wa watoto wetu wataumwa kwa kiasi kidogo sana. Na pia uwezo wa kugundua magonjwa na kuyatibu kwa uharaka utaongezeka.
Baada ya Priscilla Chan kuongea ndipo ilipofika zamu ya Mark Zuckerberg, yeye kwa upande wake alisema kuwa kwa sasa plani yao kubwa ni kufuta au kuteketeza magonjwa ya moyo, maambukizi, kansa na magonjwa ya ubongo kwani kwa sasa ndiyo ambayo yanaongoza kuleta vifo duniani.
Mark anaamini kabisa kuwa hili linawezekana lakini cha msingi ni kwamba watu inabidi wawe na subira pia wawe wavumilivu wakati wao wanafanya machakato mzima.
Mpango huu uliaanzishwa kwa mara ya kwanza mwezi septemba mwaka jana (2015) na Mark na mkewe Chan na bado unaendelea mpaka sasa
Ningependa kusikia kutoka kwako niambie hii umeipokeaje hapo chini sehemu ya comment. Inapendeza sana kuona matajiri wanatujali sio?