Facebook imeshutumiwa kutoa idadi isiyo kweli ya watu waliotazama video katika mtandao huo katika kipindi cha miaka miwili.
Facebook’s analytics ni kigezo wanachotumia wafanyabiashara wanaotangaza biashara zao kubaini ni kiasi gani video zao zinatizamwa kwenye Facebook. Mtandao huo wa kijamii unasema makosa hayo yamerekebishwa na hayajabadili kiwango wanacholipa wafanyabiashara kutangaziwa biashara zao.
Mteja mmoja anayetangaza biashara katika mtandao huo amesema kwa wakati mwingine, takwimu hizo zilipitishwa kwa hadi 80%.
Kifaa hicho cha kuhesabu kimebadilishwa jina kwa sasa na kimepewa jina “Average watch time” na Facebook imeanza kukitumia kukusanya takwimu za watu wanaotizama video mwishoni mwa mwezi Agosti.
Jarida la Wall Street limeinukuu kampuni ya Publicis iliosema kuwa Facebook kutoa takwimu za makosa “hazikubaliki”. Publicis imesema inaonyesha haja ya kuwa na kampuni ya tatu kuangalia upya takwimu zinazokusanywa na Facebook.