Utunzaji wa vitu kadha wa kadha ni muhimu sana katika maisha yetu ya kila siku na kadri siku zinavyozidi kwenda njia mbalimbali zinaibuliwa; unaweza kupata dondoo mbalimbali zinahusiana na mazingira, chakula, n.k kwenye app.
Kuna njia nyingi za kuepuka kuharibu chakula na kutokana na ukuaji wa teknolojia app mahususi imeundwa kwa ajili ya watu wote. App ya Go Green inamuwezesha mtumiaji kuweza kupata dondoo (tips) ya jinsi gani mtu anaweza akapungunguza uharibifu wa chakula. Kwa jindi ninavyoona app hii inamfaa yeyote yule hasa migahawa, hoteli, n.k.
Jinsi app hiyo inavyofanya kazi
Kila mara unapofungua app hiyo (Go Green) inakuletea dondoo mbalimbali ya jinsi ya kutoharibu chakula chako, mambo ya kuzingatia wakati wa kununua kompyuta, n.k. Dondoo zote zinahifadhiwa na kadri unavyozidi kuifungua app hiyo ndipo unapozidi kupata dondoo nyingi zaidi na kupanda daraja (rank). Ni rahisi kutoka kwenye daraja la Green Friend na kuwa Green Lover. App hiyo pia inakupa dondoo mbalimbali zitakazokusaidia kutunza mazingira.
Mafanikio
Go green app iliweza kusdhika nafasi ya pili katika shindano la “Technovation Challenge 2016” lililofanyika San Francisco, California ikifungana nafasi hiyo na wanafunzi kutoka Kenya wakijulikana kama Team Sniper.
App hiyo inapatikana katika simu zinazotumia Andrioid pamoja na iOS. Pia unaweza ukazipakuwa kwenye kompyuta, tableti, n.k.
Download | Google PlayStore (Android) . AppStore (ios)
Je, unadhani unaweza ukamshawishi na mwingine aweze kupakua app hii katika kifaa anachotumia? Tupe maoni yako na mshirikishe na nweingine.
Vyanzo: kuchwanya.com, AppAdvice