Twitter bado haijakata matumaina kabisa kama tulivyokuwa tunazani. Kwa sasa wameona bora kupitia tena ofa walizoletewa na watu ambao wanataka kununua mtandao wa Vine
Ofa hizo kama zitakuwa na faida kwao basi itakuwa ni jambo la busara kuuza mtandao huo kuliko kuacha kuendelea kuutumia.
Taarifa zilizotoka ni kwamba kampuni la Twitter limepata ofa nyingi sana za makampuni mengine kutaka kununua mtandao huo wa Vine, ofa hizo nyingi zilitoka katika makampuni mengi kutoka bara la Asia.
Japokua hakuna ushaidi wa moja kwa moja lakini inasemekana moja kati ya makampuni ambayo yalionyesha nia hiyo ni pamoja na kampuni ya Line, ambayo inajihusisha na mambo ya magemu na meseji huko nchini Japan.
SOMA PIA: Kifo Cha Mtandao Wa Vine Ndio Hiki!
La kushangaza ni kwamba japokuwa makampuni mengi yameonyesha nia lakini hakuna kampuni hata moja ambalo limetoa ofa ambayo inazidi dola milioni kumi za kimarekani. Kumbuka Twitter ilisema itaachana kabisa na mtandao huo bila hata ya kufikiria kuuza.
Pengine hilo ndio jambo ambalo limewafanya watu watake kuununua japokuwa hata kwa kiasi kidogo. Lakini swali bado linabaki pale pale, je kampuni itakubali ofa hizo (licha ya kuwa ni ndogo sana).
Kwa mtazamo mwingine ni kwamba bado kampuni la Twitter linaweza likapata faida endapo litapata mnunuzi mzuri wa mtandao wa Vine ambaye atauendeleza na kisha Twitter itakua inafaidia pale mtu anapo’share’ kitu chake katika mtandao wa Twitter (yaani ule muingiliano wa Vine na Twitter).
Ningependa kusikia kutoka kwako, je wewe unahisi Twitter itauza kweli mtandao wake wa vine au mtandao utakufa tuu kama kawaida inavyodhaniwa? Niandikie hapo chini sehemu ya comment.