NVIDIA inafanya majaribio ya magari yanayojiendesha yenyewe

0
airtel hatupimi bando
Sambaza upendo πŸ™‚
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  

Inaonekana teknolojia ya magari yanayojiendesha yenyewe inavutia makampuni mengi zaidi kwa sasa. Kampuni ya NVIDIA inafanya majaribio ya magari hayo pia katika jiji la Calfornia nchini Marekani.

NVIDIA ni kampuni kongwe katika masuala ya teknolojia za kielektroniki – wakiwa maarufu zaidi kwa teknolojia ya kadi za kigraphiki zinazotumika kwenye mamilioni ya kompyuta duniani kote (Graphic Cards).

NVIDIA inafanya majaribio ya magari

Vyanzo mbalimbali vimesema kikubwa kwa NVIDIA sio lengo la kuingia kwenye biashara hiyo moja kwa moja kwa kutengeneza magari hayo ila ni kwamba wanajikita katika utengenezaji wa teknolojia mbalimbali muhimu (kama vile processors) zinazotumiwa na magari yanayojiendesha.

Kwa sasa wameingia ubia na kampuni ya nchini China, Baidu, katika kuwawezesha kufanyia majaribio teknolojia mbalimbali wanazozitengeneza.

Makampuni yaliyojiingiza kwenye utafiti wa magari yanayojiendesha yenyewe ni pamoja na Google, Honda, Ford, Mercedes, BMW, Apple, na mengine mengi. Wengi wanapenda kwenda kufanyia majaribio magari yao katika jiji la Colifornia kwa sababu jiji hilo linasheria rafiki zaidi kwa magari yenye teknolojia ya kujiendesha yenyewe.

Tazama video inayoonesha mfumo wa kisasa kabisa wa teknolojia yao. Gari linalotumia teknolojia ya NVIDIA litaweza kujifunza zaidi kila linavyotembea zaidi.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTube,Β Telegram naΒ Google Plus

Vyanzo: Engadget na mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza upendo πŸ™‚
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  
 •  

ZINAZOHUSIANA

airtel hatupimi bando
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com