Je kuna sababu ya wewe kuziba kamera ya kompyuta yako, yaani webcam? Sababu ipo, mambo mengi yametokea ndani ya miaka kadhaa sasa yanayoonesha na kwa namna gani watu wanaweza kukuchunguza kwa kutumia webcam ya kompyuta yako.
Fahamu kuhusu Blackshades RAT
Blackshandes RAT ni programu inayomilikiwa na maelfu ya watumiaji na ni programu spesheli iliyotengenezwa kwa ajili ya kuwasaidia wadukuzi kuweza kuchunguza kompyuta za watu wengine walio maelfu ya kilomita kwa njia za mtandao. Wadukuzi wanaweza kuiba mafaili, kutumia kamera na mic ya kompyuta waliyofanikiwa kuidukua.
Mmoja wa watu waliohusika na utengenezaji wa programu hiyo tayari ashachukuliwa hatua za kisheria mapema mwaka huu lakini hili halijazuia wengine wengi kuendelea kuitumia.
Picha za uchi za Miss Teen USA
Kijana mmoja mdogo, Bwana Jared James Abrahams alikamatwa na kufunguliwa mashtaka baada ya kufanikiwa kupata picha za uchi za mshindi wa shindano la Miss Teen USA huko Marekani. Na alitumia programu ya Blackshades RAT kufanikisha udukuzi wake.
- Alimtumia binti huyo barua pepe iliyomrubuni kupakua programu ya Blackshades RAT bila kufahamu.
- Moja kwa moja kijana huyo aliweza kupata uwezo wa kuona mambo yote moja kwa moja kupitia webcam ya mdada huyo kwa miezi na miezi. Hili lilimuwezesha kumpiga picha za uchi binti huyo pale alipokuwa mwenyewe chumbani n.k,.
- Tayari watu wengi washakamtwa nchini Marekani na barani Ulaya kwa matumizi ya programu hii.
Pia kuna suala la wadukuzi wa kiserikali – kama vile NSA/CIA
Pia kuna wanaofanya uamuzi wa kuziba eneo la Webcam kutokana na kutaka kuepuka udukuzi unaofanywa na vyombo vya kijasusi vya kimataifa kama vile CIA. Katika data zilizowekwa wazi na mmoja wa watu waliokwisha fanya kazi na mashirika kama NSA/CIA, Bwana Snowden alisema mashirika hayo yanateknolojia kubwa zinazowezesha kudukua kwa urahisi vitu kama kompyuta au simu za mamilioni ya watu duniani.
Fahamu mara nyingi watumiaji wa Blackshades RAT baada ya kufanikiwa kupata picha za uchi za mtu basi uanzisha utapeli wa kutishia kuziweka wazi mitandaoni kama mtu hatatuma zingine au ata pia kama hawatapokea malipo flani.
One Comment
Comments are closed.