Umoja wa Ulaya kuipiga faini Facebook. Bodi ya usimamiaji wa ushindani barani Ulaya, Chini ya Umoja wa Ulaya (EU) limewatia hatiani Facebook kwa kosa la kuwadanganya katika hatua za uchunguzi uliowapa ruhusa ya kununua WhatsApp.
Katika moja ya hatua zilizohakikisha Umoja wa Ulaya unatoa ruhusa kwa Facebook kukamilisha ununuaji wake wa huduma ya WhatsApp ilikuwa ni kigezo cha wao kuwaambia wazi ni jinsi gani wataendelea kutumia data za watumiaji wa huduma hiyo. Kipindi wanapewa ruhusa walidai hawana uwezo wa kuunganisha taarifa na kuwatambua watumiaji wa WhatsApp na Facebook kupitia taarifa za kidata…lakini hili wameweza lifanya kwa sasa.
Mwezi wa 8 mwaka 2014 Facebook waliiambia bodi hiyo ya Ulaya kwamba haiwezekani kabisa kuunganisha taarifa ya mtumiaji mmoja wa WhatsApp na akaunti yake iliyo Facebook – hili ni jambo ambalo lilichangia wao kupewa ruhusa ya kuinunua WhatsApp… Ila miezi michache iliyopita walikuja na mabadiliko WhatsApp yanayotuma data za WhatsApp kwenda Facebook.
Kwa kiasi kikubwa chombo cha masuala ya kibiashara cha Umoja wa Ulaya kinaona Facebook walificha uwezo huo kipindi kile kwani waliogopa kama chombo hicho kingefahamu basi ununuzi wao wa WhatsApp ungepingwa katika bara la Ulaya.
Bodi hiyo ya biashara ya bara la Ulaya imesema Facebook walitoa taarifa ‘zisizokuwa za ukweli/yaani uongo’ katika kipindi cha uchunguzi ambao ulifanyika ili kujiridhisha ununuaji wa WhatsApp usingeleta madhara kwa watumiaji wa huduma hiyo.
Soma pia:
- Jinsi ya Kuikatalia WhatsApp kutuma data zako kwenda Facebook
- Facebook marufuku kuchukua data za watumiaji wa WhatsApp Ujerumani