Hakuna mtumiaji wa simu janja duniani asiyetumia programu tumishi (apps) katika simu yake na hii ni kwa sababu tunahitaji programu tumishi ili kuweza kutumia simu zetu vizuri zaidi.
Katika taarifa zilizotoka hivi karibuni katika mitandao kama vile Telegram, Amnesty International zimetoa takwimu kuhusiana na programu tumishi zilizo na ulinzi zaidi kwa mwaka 2016. Lakini unaweza ukawa unajiuliza Programu tumishi ni nini?
Programu tumishi au apps kama wengi wetu tulizoea ni programu fulani unaweza kutumia kwenye simu au kompyuta katika kufanikisha jambo fulani.
Mfano wa apps ni Facebook Messenger, WhatsApp, Gmail, GDrive, n.k.
Orodha ya programu tumishi/apps zilizo na usalama zaidi kulingana na kampuni inayoimiliki/inayozimiliki
-
Facebook
Facebook inamiliki programu tumishi mbili; WhatsApp na Facebbok Messenger. WhatsApp ambayo hivi sasa inashikilia namba moja kwa kuwa app ambayo ina ulinzi wa kutosha; mazungumzo baaina ya mtu na mtu au mazunguzo ya kwenye group yanabaki kuwa kati yenu wawili.
Facebook Messenger si salama sana kwa sababu yenyewe haina feature ijulikanayo kama end-to-end encryption. Apps hizi 2 kwa ujumla zina watumiaji zaidi ya bil. 2.
Ilipata kura 73/100
-
Apple
Kampuni hii yenye kumiliki iMessage na Facetime yenyewe imeshika nafasi ya pili katiaka orodha ya apps zenye uinzi wa kuaminika kwani apps hizo 2 haziwezi kuonyesha taarifa kwa mtu asiyehusika (iwapo app ikidukuliwa) hakuna atakayeweza kuelewa isipokuwa Apple wenyewe. Hata hivyo apps hizi zimetakiwa kuwaeleza watumiaji wote ni muda taarifa zao zinakuwa salama na ni wakati hazipo salama mathalani iwa mtu atatuma ujumbe kwenda kwa mtu asiyetumia iPhone.
Ilipata kura 67/100
-
Telegram
Telgram in app ambayo ilikuwa ya kwanza kuwezesha watu kutuma nyaraka katika mfumo wa “.doc” kabla ya app nyingine yoyote kuiga kitu hicho. Cha kushangaza ni kwamba Telegram ile feature ya ‘end-to-end encryption’ sio ya papo kwa papo (default); huwezi kujua ni wakati gani taarifa zalo zipo salama.
Ilipata kura 67/100
-
Google
Google ambao ni wamiliki wa programu tumishi Allo, Duo na Hangouts. Ukiwa na Allo app basi mawasilisno yataabaki kuwa baina yenu mnaowasiliana tu huku kwenye Duo ni chagua lako kukubali end-to-end encryption au kukataa. Hangouts haina end-to-end encryption kwahiyo si salamasana kwani taarifa zako hazijafichwa.
Ilipata kura 53/100
-
Line
Line iliyo maarufu sana nchini Japan, Indonesia, Thailand na Taiwan yenye watumiaji zaidi ya 200 milioni kila siku. Hii ni programu tumishi maarufu sana katika nchi hizo kwa sababu usalama wa taarifa za watumiaji wake unatunzwa bila ya mtumiaji kuwaza iwapo taarifa zake zipo salama au la! Na haitoi taarifa kwa mtu yeyote au kwa serikali iwapo zikihitajika.
Ilipata kura 47/100
-
Viber
Viber ni app inayofanana sana na Sype; unaweza ukatuma msg, ukapiga simu kwa njia ya video au kawaida kwa kutumia intaneti, ukapiga simu kwa mtu yoyote kwa kulipia kiasi fulani cha pesa. Ina watumiaji takribani 750 millioni na zaidi ya watumiaji 200 milioni kwa siku. Usalama wa taarifa za watumiaji wake unatunzwa bila ya mtumiaji kuwaza iwapo taarifa zake zipo salama au la!
Ilipata kura 47/100
Apps nyinginezo
Kakao ni app inayomilikiwa na kampuni moja nchini Korea Kusini na ina watumiaji hai 49 milioni kila mwezi. Skype ambayo ipo chini ya Microsoft tangu mwaka 2011 ina watumiaji zaidi ya milioni 300. Snapchat nao hawapo mbali kwani wana watumiaji milioni 100 kwa siku ingawa hawajaweka ulinzi madhubuti katika kutunza taarifa za wateja wake.
BlackBerry inafunga orodha kwa app yake ya BBM yenye watumiaji takribani 100 milioni na huduma ya end-to-end encryption ni kwa kulipia tu (sio bure).
Ni wakati wako sasa wa kuchagua app gani ya kuendelea kutumia na ni ipi ya kuachana nayo. Una mtazamo gani kuhusiana na hili. Niandikie katika sehemu ya maoni hapo chini.
Vyanzo: Amnesty International, Telegraph
One Comment
Comments are closed.