Apple ambao wanasifika kwa kutoa vitu vya bei ghali na hata apps zao kupakuliwa kwake mpaka ulizipie hivi karibuni wamezindua programu tumishi iitwayo Clips mahususi kwa ajili ya kutengeneza video na picha kwa ajili ya kutumika kwenye mitandao ya kijamii kama vile Facebook na Instagram.
Clips ambayo inategemewa kuleta ushindani katika soko la apps kutokana na mazuri na urahisi wa kutumia app hiyo ukizingatia wamelenga zitumike kwenye zile apps pendwa nikimaanisha Facebook na Instagram.
Sifa za Clips
Clips pia inampa mtumiaji urahisi wa kuunganisha picha, video fupi(clips), muziki na kufanya kuwa video na kuweza kuwashirikisha wengine kupitia app ya ujumbe mfupi wa maneno kutoka Apple au kushare kwenye Istagram, Snapchat au hata Facebook.
Kwenye app ya Clips kuna kipengele cha Live Titles kitakachowezesha kueleza video hiyo inahusu nini; itakuwa na kicha cha habari.
Clips itaanza kupatikana kwenye App store mwezi Aprili na itapatikana bila malipo. Inafanya kazi vyema kwenye iPhone 5s na matoleo mengineyo pamoja na matoleo mbalimbali ya iPad.
Vyanzo: Telegraph, pamoja na mitandao mbalimbali