Kila pale WhatsApp wanapofanya maboresho (update) ya App yao kwa watumiaji wa kawaida huchukua muda kuwafikia. Au wanapofanya majaribio ya kitu kipya katika App hiyo kwa watumiaji wa kawaida pia huwa ngumu kuwafikia.
Maboresho mapya au majaribio huwa kwa watumiaji wa Iphone tu ambao hutumia Mfumo endeshaji (Oparating system) wa iOS.
Mabadiliko hayo huwa yanaanza kwa watumiaji wa simu za mfumo endeshi wa iOS kwa simu za iPhone na baada ya mwezi mmoja ama zaidi huanza kwa simu za Android.
Lakini kuna njia ambayo itakufanya mtumiaji wa Android kuwa mtumiaji wa kwanza zaidi kupata Update zote na kwa wakati kama utaifanya.
Na njia yenyewe ni kuwa WhatsApp tester (Mtumiaji wa matoleo ya majaribio ya WhatsApp)
- Faida yake ni kwamba update zote au majaribio utapata na utaweza kuzitumia kama miongoni mwa watu wa kwanza kama watu wanaotumia mfumo wa iOS.
- Ukiwa WhatsApp tester utapata update nyingi mapema zaidi ambazo WhatsApp wanakuwa wanazitoa mara kwa mara.
Njia hii, WhatsApp wameweka ili kupata maoni ya watu kuhusiana na uzuri au ubaya wa Updates zao kabla ya kuwafikia watumiaji wake Dunia nzima.
Fata maelekezo haya ili uwe WhatsApp tester
- Ingia Google Search
- Kisha andika whatsApp Beta
- Fungua ya kwanza kabisa iliyoandikwa WhatsApp beta Tester- Google Play
- Utapelekwa katika Page ambayo itakuwa imekuingiza kuwa WhatsApp Tester
- Baada ya hapo unaweza kufungua WhatsApp yako na kushuhudia Update zote pindi zikiwekwa na kuweza kuzitumia.
- Muhimu angalia kama unahitaji Ku upadate na ufanye hivyo kwa kuingia Google Playstore.