Wengi wetu tunatumia Instagram kwa maelengo mbalimbali kama kibiashara, kujua yanayoendelea kutoka kwa watu mbalimbali, n.k ila uwezo wa kupakua kile ambacho umekiweka tumegundua si wengi wanafahamu au hata kama inawezekana.
Tunajua njia zipo nyingi ila leo fahamu moja ya njia za ku download video za Instagram
Kile ambacho unakiweka kwenye instagram iwe picha/video inawezekana kabisa kukipakua na ukawanacho kwenye simu yako kama ulikiondoa kwa bahati mbaya kwenye simu yako. Ni muhimu kuhakikisha kuwa simu yako ina nafasi ili kuweza kupakuwa kitu unachotaka kutoka Instagram.
Jinsi ya kupakua picha au picha jongefu kutoka Instagram
- Pakua programu wezeshaji ijulikanayo kama RapidSave; ni bure (haiuzwi).
- Fungua Instagram kisha nenda kwenye picha/video unayotaka kuipakua. Nakili link ya picha au video ambayo unataka uiapkue kutoka Instagram.
-
Fungua app ya RapidSave kisha paste ile link uliyocopy kutoka Instagram. Baada ya kupaste link bofya Preview halafu bonyeza Save.
- Ingia kwenye Gallery kuweza kuona picha/video uliyoipakuwa kutoka Instagram.
Kwa uwezo wa teknolojia karibu kila kitu kinawezekana na endelea kutumia Instagram katika manufaa yako na wale wanakufuatilia kwenye Instagram. Je, kuna njia gani zingine huwa unazitumia?
Play Store: RapidSave|App Store: RapidSave
Vyanzo: iDownloadBlog, mitandao mbalimbali
One Comment
Comments are closed.