Tafiti zinaonyesha kuwa iwapo mtu atatumia simu janja akiwa gizani (taa ikiwa imezimwa) na akiwa amejilaza kitandani anaweza kupofuka macho.
Imeonekana kuwa utumiaji wa simu janja gizani kwa mfano iwapo taa ikiwa imezimwa na umejilaza kitandani utaweza kupata upofu wa muda (kupoteza uwezo wa kuona kwa hadi dakika 15) na kama utaendeleza sana tabia ya utumiaji huo na usipopata matibabu sahihi unaweza tatizo hilo linaweza likawa ni la kudumu.
Wagonjwa wawili walipatwa na tatizo hilo na baada ya kufanyiwa vipimo vyote ikiwemo kipimo cha moyo na MRI hawakupatikana na tatizo lolote. Walipelekwa kwa mtaalamu wa macho na kuulizwa nini walikuwa wakifanya wakati tatizo hilo likiwatokea na kusema walikuwa wakitumia simu gizani wakiwa wamejilaza kitandani.
Ugonjwa huo kitaalamu unajulikana kama “Transient smartphone blindness” ambapo wagonjwa ni watu walikuwa wakitumia simu zao wakiwa wamejilaza kwenye mto jicho moja liikiwa limefunikwa na mto na kutumia jicho moja kuangalia wakati wakitumia simu gizani.
Daktari alishauri iwapo mtu akiwa anatumia simu gizani atumie macho yote mawili kuangalia kwenye kioo cha simu kwani atakapokuwa anatumia jicho moja na kuacha kutumia simu kisha kutoka kwenye giza, lile jicho ambalo lilikuwa limefunikwa na mto itachukua muda mpaka jicho lile kuweza kuona tena kwani tayari linakuwa limeshazoea giza.
Je, na wewe ni mmoja kati ya wale wanaopenda kutumia simu gizani? Ninaamini makala hii imekufundisha kitu. Tupe maoni yako kwa kuacha comment yako hapo chini. Endelea kuhabarika kupita Teknokona.
Vyanzo: Tech times, The Globe and Mail, theguardian
One Comment
Comments are closed.