Teknolojia ni suala linalokuwa kila siku na kama ukitaka kuwa mtaalamu katika masuala ya teknolojia huna budi kuwa mtu wa kupenda kujua kuhusu mambo mapya yanayotokea kila leo katika suala zima la teknolojia.
Satelaiti ambazo zinasaidia katika mambo mbalimbali huko angani sasa mapya yametokea katika uundaji wa satelaiti. Kijana mmoja nchini India ameunda kile kinachotajwa kuwa setilaiti ndogo zaidi ambayo itawekwa kwenye mzingo wa dunia katika kituo cha shirika la safari za anga za juu la Marekani NASA mwezi Juni.
Kifaa hicho kilichotengenezwa na kijana wa miaka 18, Rifath Shaarook cha uzito wa gramu 64, kilichaguliwa kama mshindi wa shindano lililodhaminiwa na NASA.
Soma pia: India katika masuala ya anga
Satelaiti hiyo ilichaguliwa kutoka shindano kwa jina Cubes in Space, lililoandaliwa na NASA pamoja na kampuni ya elimu ya Idoodle. Setilaiti hiyo itasafiri kwa muda wa dakika 12 katika mazingira sawa na ya angani.
Satellite hiyo imepewa jina KalamSat, baada ya jina la rais wa zamani wa India Abdul Kalam, ambaye ni mwanzishi wa miradi ya anga za juu ya nchi hiyo.
Chanzo: BBC