Skype ni mtandao wa maswala ya kupiga na kupokea simu kwa kutumia huduma ya mtandao. Pia katika mtandao huo unaweza ukafanya mambo mengine kama vile kutuma na kupokea ujumbe wa maandishi.
Kwa upande mwingine mtandao wa Snapchat umekua na mafanikio makubwa na umaarufu wa hali ya juu na jambi hili limeifanya mitandao mingine kuumiza kichwa na katika kuhakikisha wanakuja na njia kabambe za kuushinda mtandao huu.
Skype ni mtandao kabambe lakini kwa siku hizi upo kama unapotelea hivi? hii kampuni ya Microsoft imeliona na ndio maaana wako tayari kufanya maboresho makubwa (kutengeneza upya) mtandao huo.. Na kwa sasa ni kwamba mtandao unaweza ukatengenezwa kwa kufuata nyayo za Snapchat.
Maboresho makubwa mapya ambayo yanatolewa macho yanajulikana kama ‘Highlight’ na ‘Capture’ .
Capture itamuwezesha mtumiaji kupiga picha na video ambazo wanaweza kuzi’share na marafiki (contact) ndani ya Snapchat.
Highlight ni pale picha na video zitakuwa zinaonekana katika ukurasa wa mtu husika. Hii itawezesha watu kujua ni kitu gani mtu anafanya kwa siku hiyo …. Kidogo inafanana kama Stories.
Microsoft kwa upande wao hawakukataa kama wameigilizia jambo hili kutoka kwa mtandao wa kijamii maarufu wa Snapchat
Snapchat ilianzishwa mwaka 2011 na ukawa na umaarufu mkubwa ndani ya kipindi cha muda mdogo sana.