Google imekuja na njia mpya ambayo inawezesha makampuni kupata wafanyakazi kwa urahisi kabisa. Google Hire inakua inahifadhi taarifa kama zile za mawasikiano, CV na mengine mengi kutoka kwa waombaji wa nafasi za kazi.
Google Hire ni njia rahisi ya kutafuta vipaji (wafanyakazi bora) na vile vile kuweka mahusiano mazuri kati ya mwombaji kazi na mtoaji kazi.
Vile vile Google wanasema kuwa taarifa ambazo mwajiri ataweza kuaziona ni zile tuu ambazo mtafuta ajira atakubali zionyeshwe. Google Hire itafanya kazi na G Suite (amabyo ina vitu kama G maill, Google Callender n.k)
Google Hire Itakuwa Na Mambo Haya.
- Kuwa na mawasiliano kati ya pande mbili kwa kutumia Gmail au Google Hire.
- Kupanga ratiba ya mahojiano (interview) na taarifa za mahojiano hayo ndani ya Google Hire
- Waajiri wanaweza wakajua chimbuko la wafanyakazi wao (Uzoefu wa kazi) kwa kwa kutumia Google Hire
Kumbuka ni mwezi wa tano tuu hapo mtandao wa Google ulikuja na Google For Jobs ambayo hii ni msaada mkubwa kwa wale ambao wanatafuta kazi. Hii ni msaada mkubwa kwa wale wanaotafuta kazi na wale wanaotoa kazi hizo.
Google imejitetea na kusema kuwa Hire ina utofauti mkubwa sana na mitandao mingine kama vile LinkedIn kwani Hire inatumia G Suite.
Kama ni mtumiaji mzuri wa G Suite na unatafuta kazi basi huna budi kuingia katika Google Hire .