Teknolojia ya roboti ambayo kila mara ina mengi ya kushangaza dunia mathalani roboti kutomika kwenye mapokezi hospitalini, roboti mwenye uwezo wa kupika ‘burger’, n.k. Sasa wataalamu wa kutengeneza roboti wanafikiria kuja na roboti mwingine atayekuacha mdomo wazi.
Roboti atakayeweza kushiriki tendo la kujamiana: Hili jambo limewagawanya watu wengi, tayari kuna midoli (wanaserere) inayotumiwa na watu kwa tendo la kujamiiana na sasa inaonekana watu wanataka kuyapa uwezo wa kiroboti zaidi na hivyo kuwa na akili na uwezo wa kujenga uhusiano kabisa.
Kuna ule usemi unaosema “Ukistaajabu ya Mussa utaona ya firauni”, basi kama mdau wa teknolojia nathubutu kusema usemi huu kwenye makala hii umetimia. Usishangae kuona miaka kadhaa ijayo roboti atayekuwa na uwezo wa kufanya mapenzi 😯 😯 .
Nini chanzo cha uvumi huo?
Katika mkutano wa pili uliofanyika katika chuo kikuu cha Goldsmith mjini London baada ya serikali ya Malaysia ambayo ndio iliyokuwa taifa mwandamizi wa mkutano huo kuupiga marufuku. Hata hivyo, hakukuwepo na wawakilishi kutoka kwa sekta ya ngono wala roboti za ngono katika mkutano huo.
Kampuni ya Real Dolls inayotengeza wanaserere wa ngono ilidai kwamba itatengeza roboti wa ngono aliye na akili bandia mwaka ujao na iwapo uzinduzi huo utafanyika utakuwa ushahidi wa David Levy ambaye amekuwa akitabiri ujio wa roboti zinazofanana na binadamu zenye akili bandia.
Katika kipindi cha miaka 10 ijayo, inawezakana kutengeza roboti ambayo watu wataihitaji kama mpenzi, yenye upendo, kuaminika, heshima na hailalamiki. Wengi watapendelea uhusiano huo wa roboti na huenda wakataka kufunga nao ndoa.
Kuna maswali mengi ambayo majibu yake yakastaajabisha mfano ungefunga ndoa na roboti? Na je, roboti anaweza kuwa na haki ya kupinga ndoa hiyo? Tuandikie maoni yako hapo chini.
Vyanzo: BBC, mitandao mbalimbali