Nokia ni simu ambazo zilipata umaarufu sana hapo mwanzo na kuwa ndio namba moja kama simu zinazopendwa sana duniani.
Licha ya Nokia kuuza sana. simu hizi zilipotea baada ya kampuni kuuza leseni yake kwa kampuni ya Microsoft. Ukiachana na hayo, tunajua kabisa kuwa kwa sasa kampuni imerudi na imekuja na simu nyingi ambazo zinaendeshwa na programu endeshaji ya Android
Matoleo mengi yameshatoka na kwa sasa taarifa zilizopo ni kwamba toleo la Nokia 8 lipo njiani. Inategemewa kuwa Nokia 8 iwe ni toleo bora zaidi katika simu za Nokia ambazo tayari zimeshatoka.
Nokia kwa hali na mali inaonekana dhahiri kuwa wanapambana ili kuhakikisha kuwa wanakaa katika moja ya nafasi tano za juu katika watengenezaji wa simu.
HDM Global ambao ndio wamiliki na watengenezaji wa simu za Nokia wamesema kuwa wataitisha tamasha kubwa mnamo Agosti 16, 2017 ambapo ndio Nokia 8 itakapo zinduliwa.
Kwa sasa hakuna chochote cha ziada kinachojulikana juu ya simu hii isipokuwa tarehe hiyo tuu. Mambo mengi yataanza kufahamika ifikapo tarehe hiyo au kama taarifa zingine zitokee siku za usoni.