Leo fahamu jinsi ya kulogout Skype sehemu uliyoisahau au ata kama kompyuta au simu hiyo hauna uwezo wa kuifikia tena.
Ni kweli kuna mara nyingi inaweza tokea mtu kujisahau kulogout kutoka kwenye huduma unayotumia.
Kwa kifupi hawajaweka mfumo huo eneo moja kwa moja ndani ya app yake ila itakuitaji hatua fupi tuu.
Nenda kwenye mazungumzo yeyote (chat) ambayo unayo na mtu au kundi la watu ndani ya app/programu ya Skype.
- Andika
/remotelogout
- Kisha tuma
Ujumbe huu hautaonekana na mtu yeyote katika mazungumzo/chat zako na wao bali kitakachotokea ni kwamba mfumo mzima wa huduma ya Skype utalogout kwenye simu, kompyuta au tableti zingine zozote ulizokuwa umelogin bado. Itakayobakia imelogin ni hiyo tuu ambayo umeitumia kutuma ujumbe huu.
Soma makala zingine kuhusu kuhusu maujanja mbalimbali -> Teknokona/Maujanja