Kampuni ya Google imetangaza uzinduzi wa lugha 30 za sehemu mbalimbali duniani zitakazoweza kutumika katika kipengele chake cha Voice search na lugha ya kiswahili ikiwemo.
Voice search hutumika katika Android na iOS kumsaidia mtu kuweza kutafuta kitu bila ya kubonyeza au kuandika na badala yake anazungumza kwa lugha ambayo imeorodheshwa na Google.
Lugha zilizoongezwa ni;
- Amharic (Ethiopia)
- Armenian (Armenia)
- Azerbaijani (Azerbaijani)
- Bengali (Bangladesh, India)
- English (Ghana, Kenya, Nigeria, Tanzania)
- Georgian (Georgia)
- Gujarati (India)
- Javanese (Indonesia)
- Kannada (India)
- Khmer (Cambodian)
- Lao (Laos)
- Latvian (Latvia)
- Malayalam (India)
- Marathi (India)
- Nepali (Nepal)
- Sinhala (Sri Lanka)
- Sundanese (Indonesia)
- Swahili (Tanzania, Kenya)
- Tamil (India, Singapore, Sri Lanka, Malaysia)
- Telugu (India)
- Urdu (Pakistan, India)
Kuanzia sasa watumiaji wataweza kutafuta vitu kwa lugha hizo.
Lugha hizo pia zitapatikana katika Google search katika mfumo wa iOS. Kwa mujibu wa Google kutumia sauti kutafuta kitu ni njia ya kasi zaidi ya mara tatu kuliko ile ya kuandika.
Kuongezwa kwa lugha ya kiswahili na Amharic (Ethiopia) ambazo ni lugha maarufu Afrika kumeelezwa kutaongeza watumiaji wa Voice search.
Kwa miaka ya karibuni lugha ya kiswahili imeendelea kupata waongeaji wengi duniani na kuanza kufundishwa katika vyuo vikuu mbalimbali katika nchi kadhaa barani Afrika, Ulaya na Asia.