Mwaka 2014 kulikua na taarifa ambazo zilikua zinasema kuwa Google imewabidi kuwalipa apple dola bilioni moja za kimarekani ili kuwepo kama sehemu ya ‘Search engine’ katika kivinjari chake cha Safari.
Kitu ambacho google ilikua inapigania ni kuwa wakwanza katika vifaa hivyo, yaaani mtu ukiingia katika kivinnjari cha safi kutafuta kitu. Google ndio itakua inakuletea kitu ulichokitafuta na sio mtandao mwingine —Mpaka uingie katika mtandao huo moja kwa moja — wowote
Hii ilikua inawagharimu Google Dola bilioni moja za kimarekani kila mwaka. Lakini hii inaweza ikabadilika katika siku za usoni.
Japokuwa makampuni haya yana ushindani wa hali ya juu katika teknolojia zao lakini kuna baadhi ya maeneo huwa inawaladhiimu kukaa chini na kuunda ushirikiano fulani hivi.
Kwa sasa inasemekana kuwa Google itabidi iilipe Apple Dol bilioni tatu kila mwaka ili kubakia kuwa sehemu namba moja ya utafiti (Search Engine) katika vifaa vya iOS.
Hii ni hela kubwa sana lakini ukiangalia kwa upande mwingine Apple wana haki ya kuomba dau hilo. Kumbuka mambo mengi yamebadilika hata Apple mauzo yao yamepanda. HIi inamaanisha kuwa kuna simu nyingi sana za iOS ziko mikononi mwa watu na kuna nyingine nyingi tuu zitatoka.
Kumbuka hata hapo awali simu za Apple zilikua zinakuja na Apps kama Google maps na Youtube kabisa kutoka kiwandani. Lakini tangia Apple waone kuwa Google (Android) ni mpinzani mkubwa wakatoa App hizo na kuja na App kama vile Apple Maps.
Kwa haraka haraka tu ni kwamba Apple ipo katika mazingira mazuri katika mchakato huu kwani haina cha kupoteza na kuna hati hati kubwa kuwa itafanikiwa.