Kwa mujibu wa Bloomberg, kampuni ya kutengeneza vifaa vya kielektroniki zikiwemo simu za mkononi ya HTC inatarajia kuuza sehemu au biashara yake yote.
Kampuni ya HTC imejijengea umaarufu mkubwa kwa kutengeneza simu janja (Smartphones) kwa miaka kadhaa iliyopita.
Kutokana na kukua kwa ushindani kutoka kwa Samsung na Apple, kampuni ya HTC imeshindwa kujihakikishia msingi imara wa wateja hivyo kuamua kujiingiza katika ubia.
Kampuni hii pia ilipoteza maafisa wake muhimu miaka kadhaa iliyopita, akiwemo Mkurugenzi wake mkuu Peter Chou, ambaye nafasi yake ilichukuliwa na Cher Wang mnamo mwaka 2015.
Toleo la karibuni la simu za HTC ni HTC U11 ambayo imeuzwa kwa kiasi kidogo sana huko nchini Marekani.
HTC inalenga kuuza pia biashara yake ya uhalisia onyeshi (Visual Reality) ambayo kwa mujibu wa Bloomberng iliianzishwa kwa msaada wa kampuni ya Valve. Mfumo huo onyeshi wa HTC unaojulikana kama Vive unashindana vikali na ule wa Facebook wa Oculus. Hivi karibuni HTC wamepunguza bei ya bidhaa yao hii kwa bei ya dola 200 ili kuvutia wateja.
Soma pia: iPhone 6, Samsung Galaxy S6 Au Htc One M9: Simu Ipi Rahisi Kutengeneza Ikiharibika?
Hata hivyo msemaji wa HTC alipohojiwa na chombo cha habari cha CNBC, hakuwa tayari kuzungumzia swala hilo.