WhatsApp kurahisisha mawasiliano baina ya watu na makampuni mbalimbali kupitia app yao maarufu duniani.
Kampuni hiyo inafanyia majaribio uwezo wa mawasiliano kati ya watumiaji wa kawaida na makampuni au biashara kwa shughuli za kama vile mauzo na ata msaada kwa wateja.
WhatsApp kurahisisha utumiaji wa app hiyo kwa makampuni na biashara kwa ajili ya mawasiliano na wateja wao.
Kitakachotokea;
- Biashara zitapewa utambulisho rasmi (Twitter, Instagram na Facebook zinaitwa ‘verified accounts’).
- Mtumiaji wa WhatsApp wa kawaida bado ataweza kublock akaunti ya biashara kama hataki kuendelea kupata mawasiliano kutoka kwao
- Kama tayari una namba ya biashara/kampuni unayowasiliana nayo basi jina ulilotumia ndio hilohilo linakaloonekana WhatsApp ila kama hauna namba ya kampuni husika basi kwenye WhatsApp utaona jina ambalo kampuni hiyo imejiwekea lenyewe.
Hadi sasa ni biashara chache tuu zilizopewa uwezo huu, huduma hii ipo katika majaribio (beta) ila tunaamini muda si mrefu iattanza kusambaa na kuanza kutumika.